Watafiti Kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu pamoja na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya Wamefanya Ziara Mikoa Ya Nyanda za juu Kusini na mkoani Katavi

Watafiti kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA wamefanya ziara ya kiutafiti katika Mikoa ya nyanda za juu kusini na katavi ikiwa ni mwendelezo wa ziara zilizofanyika katika mikoa mingine  ili kuangalia na kuidhinisha maeneo mapya ya Utafiti wa matatizo yanayosababishwa na panya.  Watafiti hao Prof. Apia Massawe na Prof. Loth Mulungu wamesema  ziara hii imelenga katika kutimiza yafuatayo:

  1. Kutafuta maeneo ambayo yanafaa kufanyia tafiti mbalimbali zinazohusu ikolojia  ya panya kwenye mikoa husika
  2. Kuidhinisha maeneo ya tafiti kuhusiana na panya wanaopatikana kwenye mikoa hiyo
  3. Kuangalia mazingira asili kama misitu, vichaka, maeneo ya miinuko na ya tambarare ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti ili kugundua aina mpya za panya
  4. Kujionea maeneo yanayotumika kwa shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji ambapo kunatokea milipuko ya panya ili kugundua aina ya panya waliopo na kinachosababisha milipuko hiyo
  5. Kufanya utafiti juu ya magonjwa yanayobebwa na kusababishwa na panya kwa binadamu, n.k.

Watafiti wa SUA  wametembelea Mkoa Mbeya, Rukwa na Katavi na kusema kuwa tafiti zote hizi zitafanywa na Watafiti na wanafunzi wa Shahada ya Kwanza na ya pili wanaofadhiliwa na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya (ACE IRPM &BTD).

Aidha  Watafiti hao walipata nafasi ya kutembelea Ndaki ya Mizengo Pinda mkoni katavi na kuongea na wanataaluma wa Ndaki hiyo. Prof Mulungu amesema lengo kuu la kutembelea Ndaki ya mizengo pinda ni kuangalia maeneo watakayoweza kufanya tafiti kwa pamoja na wanataaluma hao na kuwashirikisha katika kusimamia tafiti za wanafunzi wa shahada ya umahili na uzamivu watakaopata fulsa ya kufanya tafiti zao mkoani katavi.

Prof. Massawe amesema ipo haja ya kuwashirikisha watafiti wachanga katika tafiti mbalimbali ili kuwa na watafiti wengi wenye mawazo chanya na walionaudhubutu wa kujifunza kutoka kwa watafiti wamuda mrefu.

Related Posts