Wananchi Wapewa Mafunzo Namna ya Kudhibiti Panya Majumbani na Maeneo Yanayozunguka Makazi Yao

Wananchi wamepewa mafunzo namna kutumia mitego ya panya ili kuzuia uharibifu ambao unaweza kusababishwa na panya hao katika mazingira wanayoishi na mazingira jirani na makazi yao.

Mafunzo hayo  yametolewa na Professa  Makundi kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA Pamoja na Prof  Steve Belmain, (Mshirika wa tafiti) kutoka  Chuo kikuu cha Greenwich Uingereza ambaye aliambatana na waandishi wa habari wabobezi katika uandishi wa habari za tafiti Chamwino mkoani Morogoro wakati  wa ziara yao katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

Wakiwa na watafiti kutoka Kituo cha Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu (INSTITUTE OF PEST MANAGEMENT) wataalamu hao walitembelea Vijiji na mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro kwa ajili kutoa mafunzo ya namna ya kudhibiti viumbe hai waharibifu wakiwemo panya.

Licha ya mafunzo hayo,Watafiti hao waliweza kutega mitego ya panya wa aina mbalimbali ili kubaini kama wanaweza kubeba vimelea vya magonjwa ambavyo vinaweza kuleta tatizo kwa wananchi waishio maeneo jirani.

Aidha,walipata wasaa wa kutembelea kituo cha Apopo.Naye Afisa Mawasiliano katika kituo cha Apopo  Bi. Lily Shalom alisema kuwa, panya huanza kupewa mafunzo baada ya wiki nne tangu kuzaliwa. Wapo panya ambao hupewa mafunzo ya kutambua vimelea vya ugonjwa wa TB na wengine ambao hupewa mafunzo ya kutambua harufu za milipuko ya mabomu.

Related Posts