Tafiti Kuhusu Panya na Magonjwa Yanayoenezwa Kutoka kwa Panya Kwenda Kwa Binadamu

Watafiti kutoka Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu wameanza kufanya tafiti katika vijiji vya Mkula, Msufini ,Sonjo na Katulakila katika Kata ya Mkula Wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro.

Tafiti za awali zimelenga kuangalia ni aina gani ya panya wanaopatikana katika vijiji hivi na aina gani ya  vimelea vya magonjwa vinavyobebwa kwenye miili ya panya ambavyo vinaweza kuambukiza magonjwa kwa binadamu. Pia wanatafiti aina ya viroboto waliopo kwa ndani aya miili ya panya ambavyo vinavinasambaza vimelea vya mgonjwa kwa binadamu pamoja na njia za kudhibiti panya na viroboto kwa kutumia mbinu za ikolojia.

Aidha Prof Makundi amesema “ Tafiti zimelenga katika kukusanya taarifa (dodoso) za matatizo mbalimbali kutoka kwa wakulima na wananchi wa vijiji husika ili kujua tatizo la panya kwa undani  na njia sahihi ya kutatua tatizo la panya kwa wakulima na afya ya jamii kwa faida ya wanakijiji na taifa kwa ujumla”.

Pamoja na hayo Prof Apia Massawe amesema ”Tafiti zimelenga katika kutatua matatizo yatokanayo na panya katika Kilimo na Afya ya jamii. Katika tafiti hizi vijiji takribani kumi na mbili vya Wilaya ya Kilombero vitafaidika na tafiti hizi.

Related Posts