Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu Yashiriki Maonesho ya Ubunifu Kitaifa

Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu Yashiriki Maonesho ya Ubunifu Kitaifa

Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu yashiriki maonesho ya ubunifu yaliyofanyika katika viwanja vya jamuhuri jijini Dodoma yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu”.

Maonesho haya yalihudhuriwa na taasisi mbalimbali na kuonyesha teknolojia mbalimbali bunifu zilizopo katika taasisi zao. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa  maonesho haya alikuwa ni makamo wa kwanza wa rais serikali ya mapinduzi Zanzibar Mhe. Othman Masoud

Katika maonesho haya ya ubunifu Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu walipata fursa ya kuonyesha teknolojia mbalimbali za ubunifu ambazo wamezigundua na zinainufanisha jamii na taifa kwa ujumla . Teknolojia hizo ni

  • Matumizi ya ndege bundi katika udhibiti wa viumbe hai waharibifu kama vile nzige,panya n.k mashambani
  • Mfumo wa kuzuia na kunasa panya kwaajili ya kudhibiti panya kwenye mashamba ya umwagiliaji mpungas Trap Barrier System(TBS)
  • Matumizi ya mkojo wa paka kufukuza panya waharibifu mashambani
  • Matumizi ya mitego kupambana na panya waharibifu majumbani na mashambani
  • Matumizi ya panya buku katika kubaini vimelea vya kifua kikuu na matumizi ya panya kuokoa waathirika wa majanga mbalimbali ardhini kama tetemeko la ardhi

Lengo kuu la maonesho haya ya ubunifu ni Kuibua, kutambua, kukuza na kuendeleza bunifu mbalimbali katika Nyanja ya sayansi na teknolojia

Related Posts