Maonyesho ya Ubunifu Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu yashiriki maonyesho ya ubunifu yaliyofanyika kampusi ya Solomon mahlangu (Mazimbu-SUA) yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu”.

Maonyesho haya yalihudhuliwa na idara mbalimbali na kuonyesha teknolojia mbalimbali bunifu zilizopo katika idara hizo. Mgeni rasmi wa maonyesho haya alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro  Mhe.Albert Msando.

Katika maonyesho haya ya ubunifu Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu walipata fursa ya kuonyesha teknolojia mbalimbali za ubunifu ambazo wamezigundua na zinainufanisha jamii na taifa kwa ujumla . Teknolojia hizo ni

  1. Matumizi ya ndege bundi katika udhibiti wa panya mashambani
  2. Udhibiti wa panya katika mashamba ya mpunga kwa kutumia njia ya Trap Barrier System(TBS)
  • Matumizi ya mkojo wa paka katika kupambana na panya waharibifu
  1. Matumizi ya mitego kupambana na panya waharibifu majumbani na mashambani

Lengo kuu la maonyeshohaya ya ubunifu ni Kuibua,kutambua, kukuza na kuendeleza bunifu mbalimbali katika Nyanja ya sayansi na teknolojia

Related Posts