Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo atembelea Banda la Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu.

Mhe. Selemani Jafo akiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taaasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai waharibifu Prof. Abdul Katakweba alitembelea banda la Taaasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai waharibifu (IPM) katika maonesho ya nanenane kanda ya mashariki 2023.

   

Katika banda letu Mhe. Waziri aliweza kupata maelezo ya namna ya kupunguza uharibifu wa mazao mashambani utokanao na panya waharibifu kwa kutumia ndege aina ya bundi. Teknolojia hii ilimshangaza sana mheshimiwa waziri kutokana na namna jamii inavyomuona ndege huyu kwa mtazamo unao husisha imani za kichawi/kishirikina tofauti na huu wa IPM wenye tija zaidi kwa mkulima katika kudhibiti panya mashambani. Maelezo yaliyotolewa kwa Waziri pamoja na watu alioambatana nao waliweza kuelewa manufaa ya ndege bundi na mchango wake katika kukabiliana na tatizo la panya waharibifu wa mazao shambani kwani anaweza kula panya mmoja hadi kumi na wawili kwa siku

   

Pia katika banda la IPM Mhe. Waziri alipata wasaa wa kujifunza na kuona faida za panya wanavyotumika kuokoa maisha ya watanzania. Aliweza kuona jinsi panya wanavyotumika kubaini vimelea vya kifua kikuu kwenye makohozi ya watu. Ilitolewa takwimu ya watanzania 29,059 ambao panya waliokoa Maisha yao wakati walipo baini vimelea vya kifua kikuu katika makohozi yao baada ya kusemekana hawana ungonjwa huo. Pia kiongozi wa APOPO kwenye maonyesho haya Pendo Msegu alieleza pia jinsi panya wanavyotumika kutambua harufu za milipuko ya mabomu. Kiongozi huyo aliendelea kumweleza Mheshimiwa Waziri kuwa kwa mwaka 2022 pekee panya hawa waliweza kusafisha eneo la mita za mraba 87,374, 285 kwenye nchi zenye matatizo ya mabomu ya kuzikwa aridhini linalo kaliwa na watu 2, 193, 278.

 

Mhe.Waziri ameipongeza SUA kwa tafiti mbalimbali na jinsi tafiti hizi zinavyoisaidia jamii ya Kitanzania. Pia amesema ipo haja ya teknolojia hizi kuwafikia watu wengi zaidi ili kutatua matatizo katika jamii.

Related Posts