WATAFITI, MKOJO WA PAKA KUIMARISHA USALAMA WA MAZAO SHAMBANI NA NYUMBANI

Watafiti kutoka Kituo cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu wamegundua njia ya kudhibiti panya kwenye mashamba na nyumbani kwa kutumia MKOJO WA PAKA. Lengo la utafiti huo ni kupunguza matumizi ya kemikali na kuongeza ufanisi katika kupunguza athari zitokanazo na panya.

Kutokana na uwezo wa mkojo wa paka kufukuza panya ndani ya nyumba na mashambani, watafiti kutoka kituo hicho wanasema kuwa kwa zaidi ya asilimia 93% panya wakihisi harufu ya mkojo wa paka hawawezi kusogea eneo husika kutokana na uadui uliopo baina ya panya na paka.

Hivyo, teknolojia hiyo itasaidia kudhitibiti panya bila kutumia kemikali ambazo zina athari kwa jamii na mazingira kwa ujumla na pia kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, kaya na taifa kutokana na kupunguza athari za panya kwenye kilimo na rasilimali nyinginezo.

Kituo cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu ni mahiri na maarufu kwa tafiti zake mbalimbali zinazolenga kudhibiti viumbe hai waharibifu kama panya, mende, dumuzi, kunguni, mbu, viroboto na papasi ambapo hadi sasa kituo kimejulikana zaidi kupitia tafiti zake za kutumia panyabuku katika kutambua uwepo wa mabomu ardhini na vimelea vya kifua kikuu.

 

Related Posts