Watafiti Kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu pamoja na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya Wamefanya Ziara Mikoa Ya Kanda Ya Ziwa

Watafiti kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya wamefanya ziara ya kiutafiti katika mikoa ya kanda ya ziwa ili kuangalia na kuidhinisha maeneo mapya ya Utafiti wa matatizo yanayosababishwa na panya. . Watafiti hao Prof. Apia Massawe na Prof. Loth Mulungu wamesema  ziara hii imelenga katika kutimiza yafuatayo:

  1. Kutafuta maeneo ambayo yanafaa kufanyia tafiti mbalimbali zinazohusu ikolojia  ya panya kwenye miko a ya kanda ya ziwa Victoria
  2. Kuidhinisha maeneo ya tafiti kuhusiana na panya wanaopatikana kwenye mikoa inayozunguka Ziwa Victoria
  3. Kuangalia mazingira asili kama misitu, vichaka, maeneo ya miinuko na y a tambarare ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti ili kugundua aina mpya za panya
  4. Kujionea maeneo yanayotumika kwa shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji ambapo kunatokea milipuko ya panya ili kugundua aina ya panya waliopo na kinachosababisha milipuko hiyo
  5. Kufanya utafiyi juu ya magonjwa yanayobebwa na kusababishwa na panya kwa binadamu, n.k.

Watafiti wa SUA  wametembelea Mkoa wa Kagera na Mwanza na kusema kuwa tafiti zote hizi zitafanywa na wanafunzi wa Shahada ya Kwanza nay a pili wanafadhiliwa  na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya.

Aidha Prof. Apia Massawe amesema kuwa kutoka na mwonekano wa ikologia ya sehemu mbalimbali za Mkoa wa Kagera,ikichangiwa pia na hali ya hewa  ambayo si joto sana, inawezekana panya waliopo wakawa  wamebeba vimelea vya magonjwa kama tauni. Katika historia ya Mkowa wa Kagera kulishatokea milipuko ya ugonjwa wa Tauni  kama miaka karne moja iliyopita. Inajulikan kuwa bakiteria wanaosabisha ugonjwa wa tauni wanaweza kuwepo wanazunguka ndani ya miili ya panya kwa muda wa miaka mingi bila milipuko  kotokea kwa binadamu. Aidha, kama kutatokea mabadiliko yanayosababishwa na shughuli za binadamu au mabadiliko yanayotokana  na tabia nchi ugonjwa unaweza kujitokeza kwa upya ndani ya jamii na kuleta milipuko kwa upya.

 

Related Posts