Ufunguzi Wa Maonyesho Ya Kilimo,Mifugo Na Uvuvi Kitaifa Yafunguliwa Rasmi 01/08/2020 Mkoani Simiyu

Maonyesho ya kilimo, mifugo na uvuvi kitaifa  yamefunguliwa rasmi na  Makamu wa Raisi Mhe Mama Samia Suluhu Hassan mkoani Simiyu. Maonyesho haya yamekuja na kauli mbiu inayosema “Kwa maendeleo ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi chagua viongozi bora 2020”.

Aidha Makamu wa Raisi ameipongeza wizara ya kilimo na uvuvi kwa kujenga jingo la kudumu katika  viwanja vya Nyakabindi vilivyopo wilayani  Bariadi mkoani Simiyu.

Amesema lengo na dhumuni la maonyesho ya Nanenane mkoani Simiyu ni kuwapa fursa wakulima,wafugaji na wavuvi kujitangaza kibiashara na kupata fursa ya kuonana na watafiti mbalimbali kupata elimu juu ya mbegu bora, ufugaji bora na uvuvi wenye tija.

Pia katika maonyesho haya Kituo cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibufu kinashiriki kuwapatia wakulima na wafugaji elimu ya udhibiti wa viumbe hai waharibifu  mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ikiwemo udhibiti wa panya mashambani  kama vile mashamba ya mpunga, maharage na mashamba ya mahindi, udhibiti wa panya majumbani na ufugaji au utunzaji wa ndege aina ya Bundi  mashambani katika kupunguza baa la panya waharibifu.

Pamoja na haya Kituo cha Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu kinatoa elimu kuhusu panya wanaotumika kubaini vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na panya wenye uwezo wa kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini kwa kunusa.

Related Posts