Taasisi Ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu Yashiriki Wiki ya Kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine.

Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibufu yashiriki Kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine inayofanyika katika viwanja vya michezo Kampasi kuu SUA kuanzia Mei 23 hadi 26. Taasisi imepata nafasi ya kuonyesha teknolojia mbalimbali katika maonesho haya.

   

Katika ushiriki wa Kumbukizi hii Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu  imepata fursa ya kuonyesha teknolojia na tafiti mbalimbali zinazofanywa katika Taasisi hii.Miongoni mwa teknolojia zinazoonyeshwa ni pamoja na;-

  1. Udhibiti wa Panya kwenye mashamba ya Mpunga kwa kutumia fensi ya kuzuia panya kuingia shambani
  2. Udhibiti wa panya nyumbani kwa kutumia mitego mbalimbali na viwatilifu
  3. Matumizi ya ndege bundi katika udhibiti wa panya waharibifu shambani
  4. Teknolojia ya kubaini vimelea vya kifua kikuu kwa kutumia panya
  5. Teknolojia ya kubaini harufu za milipuko kama mabomu kwa kutumia panya n.k

Aidha tumepata fursa ya kutembelewa na Mgeni rasmi wa ufunguzi wa maonyesho haya Mhe.Abdallah Ulega Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na viongozi waandamizi wa Chuo.Mgeni rasmi alipata wasaa wa kujifunza mambo mbalimbali katika banda la Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu kama vile matumizi ya ndege bundi mashambani na elimu kuhusu ndege huyu kwa ujumla.

   

Pia tumepata nafasi ya kutembelewa na Mkuu wa chuo cha Sokoine cha Kilimo Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Warioba.Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe hai Waharibifu Dr.Martin John alipata wasaa wa kuelezea teknolojia zote zilizopo katika banda letu.

   

Kwa mwaka 2023 maadhimisho hayo yanabebwa na Kauli mbiu isemayo, Mazingira wezeshi  kwa vijana kushiriki katika  Kilimo, sera , miongozo na utendaji, ambapo kauli hiyo  inalenga kuhamasisha vijana  kushiriki kikamilifu  katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi  kwa kuwawekea mazingira rafiki.

Related Posts