Nanenane Kanda ya Mashariki 2023 Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Morogoro

Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibufu SUA (IPM) inashiriki maonesho   ya  wakulima kanda ya mashariki katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere vilivyopo mkoani Morogoro.

Maonesho haya ya wakulima yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula”. Lengo la kauli mbiu hii ni kuhamasisha ushiriki wa vijana na wanawake katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, Ufugaji wa mifugo na uvuvi .Hii ni kutokana na ukweli kwamba  Vijana na wanawake ndio kundi kubwa sana katika jamii ya kitanzania. Kundi hili litajikita katika uzalisha chakula litaleta mafanikio makubwa kupitia kupitia klimo, ufugaji na uvuvi Tanzania.

 

Katika maonesho haya Mgeni rasmi siku ya ufunguzi alikuwa  Waziri Mkuu mstaafu awamu ya nne Mhe. Mizengo Peter Pinda ambapo aliweza  kupata wasaa wa kutembelea mabanda ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. Akiwa katika mabanda ya SUA  aliweza pia kutembelea Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibu ikiwemo APOPO  kuona teknolojia mbalimbali zinazotumika kudhibiti viumbe hai waharibifu mashambani na majumbani Pamoja na kusaidia kuokoa Maisha ya jamii.

Miongoni mwa teknolojia zinazooneshwa ni kama zifuatazo;-

         i.            Teknolojia ya udhibiti wa panya kwenye mashamba ya Mpunga

       ii.            Teknolojia ya matumizi ya ndege aina ya  bundi kupunguza panya waharibifu kwenye mashamba

     iii.            Matumizi ya mitego mbalimbali kudhibiti panya ndani ya nyumba

     iv.            Matumizi ya viuatilifu vya kuua panya majumbani

 

Aidha kwa upande wa APOPO mgeni rasmi aliweza kuona  jinsi panya wanavyotumika kusaidia jamii katika mambo mbalimbali kama vile Kutambua vimelea vya kifua kikuu kwenye makohozi ya binadamu na jinsi panya wanavyotumika kutambua harufu za milipuko ya mabomu.

 

Maonesho haya yalianza tar 1-8-2023 yanaendelea hadi tar 8-8-2023 Karibuni sana katika banda la Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu.

 

 

Related Posts