Mkutano Wa Mwaka Wa Mradi Wa Kituo Mahiri Cha Teknolojia Bunifu Za Udhibiti Wa Panya Na Uendelezaji Wa Teknolojia Za Unusaji

 

Watafiti wa Mradi wa Kituo Mahiri cha Teknologia bunifu za udhibiti wa panya na uendelezaji wa teknolojia za unusaji kushirikiana na washirika wake kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na nchi mbalimbali  wamekutana ARUSHA kwenye mkutano wa mwaka kujadili maendeleo ya mradi. Mkutano unafanyika kwenye Taasisi ya sayansi na teknolojia kuanzia tarehe 4 hadi 5 Februari 2020.

Mkutano ulifunguliwa na Mkurugenzi wa DPRTC, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Profesa Esron Karimuribo. Aidha mgeni rasmi amewapongeza viongozi wa kituo mahiri cha Teknolojia bunifu za udhibiti wa panya na uendelezaji wa teknolojia za unusaji Prof. Apia Massawe na Prof Rhodes  Makundi  kutoka kituo cha kudhibiti viumbe hai waharibifu SUA kuwa kuonesha mfano bora katika utekelezaji wa mradi huu ambao umewezesha chuo kujivunia.

Katika mkutano huo yamejadiliwa mafanikio yaliyopatikana kupitia  mradi huo ikiwemo kuweza kujenga kituo cha kufugia wadudu na mradi umefanikiwa kutoa ufadhili wa shahada za uzamili na uzamivu kwa wanafunzi 16 kwa mwaka 2019/2020 kutoka ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Idara ya Uhifadhi wa Wanyama pori katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Dr. Nsajigwa Mbije wakati akitoa ripoti ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka huu kupitia mradi huu. Dr. Mbije amesema kuwa mradi huo umefanikisha kuongeza idadi ya wanafunzi wa uzamivu katika idara hiyo ukilinganisha na mwaka 2017/2018 ambapo wanafunzi 10 pekee ndio walipata nafasi.

Aidha katika mkutano huo yamejadiliwa mafanikio yaliyopatikana kutokana na matumizi ya panya buku kutambua vimelea vya kifua kikuu. Dr .G. Mgode akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa upimaji wa kifua kikuu kwa kutumia panyabuku ambao ni sehemu ya kituo mahiri alisema kwa mwaka 2019 wafanikiwa kupima wagonjwa wengi zaidi ukilinganisha na mwaka 2018 hali ambayo alisema inaashiria kukubalika kwa teknolojia ya unusuaji kutumia panyabuku waliuofundishwa.

Mradi wa ACE II unauhusiana na mradi wa maendeleo ya teknolojia ya ubunifu wa panya katika kufanya tambuzi mbalimbali umelenga kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya tisini (90) wa shahada za uzamili na uzamivu kutoka ndani na nje ya nchi kwenye masuala ya tafiti za teknolojia mbalimbali zinazohusisha viumbehai waharifu huku nchi kama Tanzania, ubeleji, Uingereza, Ethiopia na Uganda wakiwa ndio wadau wakubwa kwenye mradi huu.

Related Posts