Mkutano wa Kaimu Mkurugenzi Wakurugenzi na Watafiti Wastaafu wa Taasisi Ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu

Kaimu Mkurugenzi Prof. Mulungu wa Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu amefanya mkutano na wakurugenzi  na watafiti wastaafu  wa taasisi hii . Mkutano huu umehudhuriwa na wakurugenzi na watafiti wote waliomaliza muda wao wa uongozi na kujadili masuala mbalimbali ya kitafiti, kitaaluma na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.

Aidha katika Mkutano huu yamejadiliwa masuala mbalimbali ikiwemo  uundaji wa idara mbalimbali, ujenzi wa majengo ya taasisi, pamoja na kuongeza idadi ya wanataaluma na wafanyakazi wawezeshaji.

Kaimu Mkurugenzi amewashukuru sana wakurugenzi  na watafiti wastaafu kuhudhuria mkutano huu Pia wakurugenzi wastaafu wameahidi kushirikiana kwa karibu na Kaimu mkurugenzi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Related Posts