Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu Ahamasisha Wafanyakazi Kupata Chanjo ya Uviko wa 19 (covid 19)

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu, Dkt. Ladslaus Mnyone ahamasisha wafanyakazi wa Taasisi na Nchi kwa ujumla kupokea huduma ya chanjo ya Uviko wa 19 kwa moyo mmoja na amani ili kuhakikisha afya njema katika kupambana na kirusi cha uviko wa 19.

Ameyasema hayo baada ya kupata chanjo hiyo katika Hospitali ya Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwenye Uzinduzi wa Huduma ya Ugawaji Chanjo ya Uviko wa 19 tarehe 4 Agosti 2021.

Huduma ya Ugawaji wa Chanjo ya Uviko wa 19 (Covid 19) imezinduliwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda huku amasa ikionekana kuwa kubwa kutokana na idadi ya ushiriki wa  watumishi wa SUA katika kupatiwa chanjo hiyo.

Tuungane pamoja katika kujali afya ya kila mmoja kwa maendeleo ya Taifa.

Related Posts