MAONYESHO YA NANENANE KITAIFA MKOANI SIMIYU

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof Florens Luoga atembelea Banda la Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) ambapo Kituo Cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu kinaonyesha tafiti na teknolojia mbalimbali na kukipongeza kituo kwa tafiti wanazozifanya kuwa na manufaa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha Gavana amesema ipo haja ya serikali kuwawezesha watafiti katika tafiti mbalimbali wanazozifanya kama vile utafiti wa kutambua ugonjwa wa kifua kikuu haraka ili kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu na kupunguza gharama zinazotumika kuwahudumia wagonjwa.

Pamoja na hayo Gavana amesema amefurahishwa na jitihada za Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo katika kuelimisha wananchi faida za ndege aina ya Bundi anayewezakutumiwa vizuri kama mojawapo ya njia rahisi za kupambana na panya waharibifu mashambani na kuachana na imani potofu wanazomuhusisha nazo ndege huyo.

Related Posts